Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yapata pigo kubwa baada ya korti kuruhusu Miguna kurejea nyumbani

6ac8c6d601f35b7f.png Serikali yapata pigo kubwa baada ya korti kuruhusu Miguna kurejea nyumbani

Mon, 7 Jun 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Serikali imepata pigo kubwa baada ya Mahakama ya Rufaa kumruhusu wakili aliyefurushwa nchini Miguna Miguna kurejea nyumbani.

Haya yanajiri baada ya jopo la majaji watatu wa Mahakama ya Rufaa Roselyn Nambuye, Wanjiru Karanja na Mohammed Warsame siku ya Ijumaa, Juni 4, kutupilia mbali ombi la Mwanasheria Mkuu Kihara Kariuki kubatilisha uamuzi wa Jaji Enock Mwita wa kuharamisha kufurushwa kwa Miguna Februari 2018.

Kwa kauli moja majaji hao walisema serikali ilishindwa kuthibitisha kuwa haikukandamiza haki za Miguna ilipofuta uraia wake ilhali alizaliwa Kenya katika eneo la Nyando, Kaunti ya Kisumu mwaka wa 1962.

"Serikali kupitia kwa Waziri wa Usalama na Masuala ya Kigeni imeshindwa kuwasilisha ushahidi kuthibitisha jinsi agizokuwa Miguna akubaliwe kurudi nchini na alipwe fidia ya Sh7.2 milioni litakavyoiathiri," majaji Nambuye, Karanja na Warsame walisema katika uamuzi wao.

Miguna alifurushwa nchini baada ya kumwapisha kinara wa ODM Raila Odinga kuwa rais wa watu.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke