Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yaongeza wanajeshi kudhibiti mapigano ya kikabila

Darful Wanajeshi Serikali yaongeza wanajeshi kudhibiti mapigano ya kikabila

Tue, 26 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Sudan limeongeza askari zaidi katika jimbo la Magharibi Darfur kwa lengo la kudhibiti mapigano ya kikabila ambayo yanadaiwa kusababisha mauaji ya watu zaidi ya 175 kwa muda wa takribani siku tano zilizopita.

Jumapili iliyopita kulitokea makabiliano makali kati ya jamii ya Waarabu na wasio Waarabu katika mji wa Kreinik, ulio umbali wa kilometa 80 mashariki mwa mji mkuu wa jimbo la Darfur, Genena. Kimsingi mapigano hayo yaliingia hadi katika viunga vya jiji la Genena, eneo ambalo kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa serikali ilitangaza marufuku ya kutotoka nje katika nyakati za usiku.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amelaani machafuko hayo ambayo yalisababishwa na kuuliwa kwa watu wawili wa jamii ya Kiarabu na wavamizi ambao hawakuweza kufahamika mara moja. Katibu mkuu huyo pia alitoa wito wa kuharakishwa kwa upelekaji vikosi vya kulinda usalama vya ndani kwa mujibu wa makubaliano ya amani ya 2020 kati ya serikali ya Sudan na muungano wa waasi katika eneo lililoharibiwa vibaya kwa vita la Darfur.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live