Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yaondoa maafisa wa polisi waliokuwa wakihudumia Moi

519d70edfc13c416 Serikali yaondoa maafisa wa polisi waliokuwa wakihudumia Moi

Fri, 30 Jul 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Njiru alisema wameagizwa kurudi katika wizara ili kutumwa kazi katika maeneo mengineInaarifiwa ni walinzi katika kaburi la Moi nyumbani kwake Kabarak ambao watasalia huku wengine wote wakirudi kambi ya GSUFamilia ya Moi imekuwa ikifurahia huduma za watumishi wa umma lakini sasa inaarifiwa bajeti ya kufadhili hilo ilisimamishwaSerikali imewaondoa maafisa wa usalama waliokuwa wakihudumia aliyekuwa rais Daniel Moi kama walinzi.

Kwa mujibu wa jarida la People Daily, mafiasa hao kutoka kikosi cha GSU wametakiwa kurudi kwenye vitengo rasmi ili kupewa kazi nyingine.

Jarida hilo lilisema ni maafisa watakaolinda kaburi lake pekee ambao wataendelea kuwa Kabarak Nakuru alipozikwa.

Kulingana na aliyekuwa karani wa mawasiliano wa Moi, Lee Njiru, mkuu wa utumishi wa umma James Kinyua ameagiza watumishi wa umma waliokuwa chini ya Moi kurudi kwenye wizara zao.



“Ni kweli maafisa hao wameondolewa. Ni agizo kutoka kwa mkuu wa utumishi wa umma Joseph Kinyua baada ya bajeti iliyokuwa imetengewa Moi kumalizwa,” Njiru aliambia jarida hilo.



Read also

Afisa wa Zamani wa GSU Miongoni mwa Waliovamia Benki ya Equity Matuu

Maeneo yaliyoathirika ni Kabarak Nakuru na Moi Gardens jijini Nairobi ambapo wafanyakazi hao walikuwa wakitoa huduma.

Moi alihudumu kama rais kuanzia 1978 hadi 2002 wakati ambapo alistaafu na chama chake cha KANU kuondolewa mamlakani.



Mzee Moi alifariki dunia Februari 4, 2020 akiwa na miaka 95 katika hospitali ya Nairobi baada ya kuugua kwa muda.

Vigogo wa kisiasa wakiongozwa na Rais Uhuru Kenyatta walikongamana nyumbani kwake Februari 12 ambapo walimpa mkono wa buriani.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsApp: 0732482690.

Tazama Video Kemkem za Kusisimua Kutoka hapa TUKO.co.ke
Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke