Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yamtimua mzabuni wa Ufaransa, uhaba wa mafuta

Mafuta Kenya Uhabaaa Mdhabuni Serikali yamtimua mzabuni wa Ufaransa, uhaba wa mafuta

Thu, 14 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mamlaka nchini Kenya imeripotiwa kufuta kibali cha kufanya kazi cha mtendaji mkuu wa Ufaransa wa mojawapo ya kampuni ya kubwa ya kuuza mafuta nchini Kenya kutokana na tatizo la uhaba wa bidhaa hiyo.

Serikali inasemekana kuamuru kufukuzwa nchini kwa Christian Bergeron, mtendaji mkuu wa Rubis Energy Kenya - kampuni tanzu ya Rubis Group yenye makao yake nchini Ufaransa.

Siku ya Jumanne mamlaka ya udhibiti wa kawi nchini humo iliwashutumu baadhi ya wauzaji mafuta kwa kuzuiausambazaji wa mafuta katika soko la ndani na kutoa kipaumbele kwa mauzo ya mafuta kwa nchi jirani.

Mamlaka hiyo aidha ilisema kampuni hizo zitaadhibiwa kwa kupunguziwa kiwango cha mafuta watakayoruhusiwa kuagiza kwa muda wa miezi mitatu ijayo.

Makampuni ya mafuta ya Kenya yanauza takriban 65% ya bidhaa zao kutoka nje kwa soko la ndani na nyingine kwa nchi jirani zisizo na bandari kama vile Uganda, Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Kumekuwa na uhaba mkubwa wa bidhaa hiyo katika wiki za hivi karibuni kote nchini, huku milolongo mirefu ya magari katika vituo vya kuuza mafuta.

Mamlaka ya Kenya inasema kuna mafuta ya kutosha katika hifadhi yake.

Kuna uvumi kwamba baadhi ya wauzaji wamekuwa wakihifadhi mafuta kwa kutarajia ongezeko la bei leo Alhamisi wakati bei za mwezi ujao zitatzngazwa.

Wataalamu wanasema mzozo wa sasa nchini Kenya umesababishwa na kucheleshwa kwa utoaji ruzuku ya mafuta inayodaiwa na wauzaji mafuta.

Kenya inatoa ruzuku kwa bei ya mafuta ili kuwakinga raia wake dhidi ya bei ya juu mafuta.

Lakini wauzaji mafuta wamekuwa wakilalamikia kucheleweshwa kwa malipo ya kufidia bei wanayotoza watumiaji inayotakiwa kulipwa na serikali kama ruzuku.

Serikali ilitoa baadhi ya malipo yaliyocheleweshwa wiki iliyopita.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live