Katika kuhakikisha huduma za mawasiliano zinasambaa nchini, serikali inakusudia kuimarisha huduma za hizo kwa kuweka mtandao wa Intaneti bure (WIFI) kwenye mikusanyiko ya watu, vyombo vya usafiri na kwenye shule, ili kila mwananchi apate huduma hiyo bila usumbufu wowote.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Methew Kundo, wakati akifungua kikao cha 41 cha Baraza la Utawala la Umoja wa Posta Afrika (PAPU).
Amesema kikao hicho kimefanyika ikiwa ni mfululizo wa vikao vyao, kwa ajili ya kuandaa ajenda ya pamoja kwa nchi za Afrika, ili kuziwasilisha katika kikao cha Baraza la Posta Duniani kitakachokaa Oktoba mwaka huu.
Mhandisi Kundo uwekaji huo wa intaneti za bure, utasaidia wananchi kupata huduma za mawasiliano popote wanapokuwa na kuendelea na shughuli zao za kijamii, bila mkwamo wa ukosefu wa huduma hiyo.
“Tunaboresha mifumo ya utendaji kazi na kua ya kidijitali na sisi kama Tanzania tukiwa wanachama wa umoja huu Afrika na Duniani, tumeanza fanya vizuri kwa kuanza na utekelezaji wa makubaliano, tuliyojiweke kwenye umoja wetu wa Afrika na Duniani, kwa kuweka sawa sera yetu ya posta ya mwaka 2003 kwa kuboresha miundombinu ya mawasialiano.”