Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yaamua kugawa Wi-Fi bure kwa wananchi

Serikali Yaamua Kuygawa Wi Fi Bure Kwa Wananchi.jpeg Serikali yaamua kugawa Wi-Fi bure kwa wananchi

Thu, 25 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali ya Uganda imesema inaongeza vituo 2,000 zaidi vya Wi-Fi ya bure kote nchini katika hatua ambayo inatajwa kuongeza ufikiaji wa huduma ya intaneti katika maeneo ya pembezoni mwa nchi, ikiwemo wakati wa dharura kwa watakaohitaji huduma za Serikali kama vile usajili wa Vitambulisho vya Taifa.

Hii ni sehemu ya mpango maalum wa kuboresha miundombinu ya mawasiliano kimikoa ambao ulianza mwaka 2016 na unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka huu utakaogharimu dola milioni 75 (sawa na Tsh bilioni 174.9).

Uwekaji wa mitambo hiyo ya Wi-Fi utafanyika katika maeneo yote muhimu ya nchi hiyo ambayo yanapitiwa na Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano.

Kwa mujibu wa mamlaka za Serikali nchini humo, wananchi wataweza kupata internet bure kwa muda maalum utakaopangwa Serikali huku Ofisi za Serikali zikitumia internet hiyo kwa kazi za Kiserikali.

“Tutatoa internet bure kwenye maeneo yaliyochaguliwa, kwa wakati uliopangwa. Internet hiyo itatumiwa na Serikali katika muda wa kazi na kwa wananchi ni baada ya muda wa kazi na weekend,” alisema ofisa mmoja wa Serikali nchini humo.

Aliongeza pia kuwa, internet hiyo itatumika katika kazi maalum na za dharura hasa katika kuomba na kutoa huduma za kiserikali kwa umma kama usajili wa vitambulisho vya Taifa.

Hadi sasa Uganda imeweka vituo 600 vya Wi-Fi katika Mikoa mbali mbali nchini humo ambapo 300 kati yao vipo Jijini Kampala.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live