Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali ya kijeshi Niger yasema rais aliyepinduliwa alijaribu kutoroka

Serikali Ya Kijeshi Niger Yasema Rais Aliyepinduliwa Alijaribu Kutoroka Serikali ya kijeshi Niger yasema rais aliyepinduliwa alijaribu kutoroka

Fri, 20 Oct 2023 Chanzo: Bbc

Serikali ya kijeshi nchini Niger imesema imezuia jaribio la aliyekuwa Rais aliyeondolewa madarakani, Mohamed Bazoum, kutoroka kizuizini.

Rais huyo wa zamani alijaribu kutoroka usiku na familia yake, wapishi na usalama, msemaji wa jeshi alisema.

Kulikuwa na mipango ya kundi hilo Kwenda nchi nyingine kwa helikopta lakini mpango huo uligundulika, aliongeza.

Bw Bazoum amekuwa chini ya kizuizi cha nyumbani tangu wanajeshi wa kikosi cha rais kufanya mapinduzi mwishoni mwa Julai.

Niger ni sehemu muhimu ya kanda ya Afrika inayojulikana kama Sahel - ukanda wa ardhi unaoanzia Bahari ya Atlantiki hadi Bahari ya Shamu. Eneo hilo linasumbuliwa na wanajihadi na limezingirwa na tawala za kijeshi.

Jaribio la kutoroka lilitokea mwendo wa 03:00 (02:00 GMT) siku ya Alhamisi, msemaji wa jeshi Amadou Abdramane alisema kwenye runinga ya serikali.

"Rais aliyeondolewa madarakani Mohamed Bazoum na familia yake, wapishi wake wawili na maafisa wawili wa usalama, walijaribu kutoroka kutoka katika kizuizi chake," alisema.

Mpango wa kutoroka ulifeli na "wahusika wakuu na baadhi ya washirika" walikamatwa, aliongeza.

Mpango huo wa kina ulihusisha Bw Bazoum kufika kwenye maficho nje kidogo ya mji mkuu Niamey, Bw Abdramane alisema.

Kundi hilo lilikuwa limepanga Kwenda nje ya nchi kwa helikopta kuelekea Nigeria, aliongeza, na kukashifu "tabia ya kutowajibika" ya Bw Bazoum.

Haijabainika ni wapi sasa rais huyo wa zamani na wengine wa kundi hilo wanashikiliwa. Uchunguzi umeanzishwa.

Jeshi la Niger lilimpindua rais aliyechaguliwa kwa njia ya kidemokrasia katika mapinduzi ya tarehe 26 Julai.

Ilionyesha uvamizi sawa wa kijeshi katika nchi jirani za Burkina Faso na Mali, huku kukiwa na uasi wa Kiislamu na ushawishi unaoongezeka wa Urusi katika eneo pana la Sahel kupitia kundi lake la mamluki la Wagner.

Bw Bazoum amekataa kujiuzulu rasmi.

Chanzo: Bbc