Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali ya Umoja ni chaguo bora zaidi - Ramaphosa

Serikali Ya Umoja Ni Chaguo Bora Zaidi   Ramaphosa Serikali ya Umoja ni chaguo bora zaidi - Ramaphosa

Fri, 7 Jun 2024 Chanzo: Bbc

Chama cha African National Congress (ANC) cha Afrika Kusini kitaalika vyama vingine vya kisiasa kuunda serikali ya umoja wa kitaifa, kiongozi wake Rais Cyril Ramaphosa amesema.

Hatua hiyo inakuja baada ya uchaguzi wa wiki jana ambapo ANC ilipoteza wingi wa viti vya ubunge kwa mara ya kwanza tangu kumalizika kwa mfumo wa ubaguzi wa rangi miaka 30 iliyopita.

Bw Ramaphosa alisema ANC ilikubali maoni ya watu, na akatoa wito wa kufanyika kwa mazungumzo ya kitaifa ili kusaidia kujenga upya mshikamano wa kijamii.

Vyama vya kisiasa vina zaidi ya wiki moja tu kuunda serikali kabla ya bunge kufanya mkutano wa kumchagua rais wa nchi hiyo.

Chini ya mfumo wa uwakilishi sawia wa Afrika Kusini, ili serikali kuwa na wingi wa uhakika itahitajika kuundwa na vyama ambavyo kwa pamoja vilipata zaidi ya 50% ya kura.

ANC ilichukua mgao wa 40%, huku chama cha mrengo wa kati cha Democratic Alliance (DA) kikipata 22%, chama cha MK cha Rais wa zamani Jacob Zuma kilipata 15% na chama chenye siasa kali za Economic Freedom Fighters (EFF) 9%.

Chanzo: Bbc