Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali ya Uganda yazifutia usajili NGO's 54

UGANDA Serikali ya Uganda yazifutia usajili NGO's 54

Fri, 20 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali ya Uganda imetangaza kuzifungia taasisi zisizo za kierikali (NGO’s) 54 ikiwa ni muelendelezo wa serikali ya nchi hiyo kuzibana taasisi na mashirika ya kijamii. Na moja kati ya mashirika yaliyokutwa na mkasa huo ni pamoja na Chapter Four.

Taarifa iliyotolewa na Mamlaka ya Usimamizi wa Taasisi hizo (NBN) ambayo iko chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchini Uganda imesema agizo hilo linatakiwa kutekelezwa haraka iwezekanavyo kuanzia sasa.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo imeelezwa kuwa sababu za kufutwa kwa NGO’s hizo ni kutokana na kushindwa kutumizi masharti na sharia za usajili zinazosimamia shughuli zote ndani ya taasisi hizo ikiwemo kufanya shughuli nje ya muda wa usajili, kushindwa kutoa taarifa za kifedha na ufadhili pamoja na kushindwa kusajili taasisi hizo.

Baadhi ya taasisi zilizofungwa ni zile zilizojihusisha na kufatilia masuala ya uchaguzi na upigaji kura mwezi Januari ambapo kulitawaliwa na vurugu na vitisho vya majeshi ya Uganda hali iliyopelekea kuwepo ukamataji wa wananchi na viongozi walioshiriki uchaguzi wa nchi hiyo.

Uchaguzi Mkuu wa Uganda umemrudisha Rais Yoweri Museveni mamlakani kwa kipindi cha sita huku kukiwa na vurugu kubwa mtaani, ukamataji wa wapinzani kubanwa kwa shughuli za wana habari na kushikiliwa idadi kubwa ya watu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live