Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali ya Uganda yatenga $800m kuwafundisha Waganda Kiswahili

Serikali Ya Uganda Yatenga $800m Kuwafundisha Waganda Kiswahili Serikali ya Uganda yatenga $800m kuwafundisha Waganda Kiswahili

Thu, 14 Mar 2024 Chanzo: Bbc

Serikali ya Uganda imetenga $800m (£625m) kukuza na kufundisha lugha ya Kiswahili nchini humo, kama sehemu ya juhudi za kuimarisha ushirikiano wa kikanda.

Watumishi wa umma wakiwemo madaktari, wauguzi na wafanyakazi wa mpakani watapewa kipaumbele katika programu ya mafunzo ya Kiswahili ambayo bado haijazinduliwa, Waziri wa Uganda wa Masuala ya Afrika Mashariki Rebecca Kadaga alisema.

Waziri hakutoa maelezo zaidi kuhusu lini na jinsi gani programu ya mafunzo itazinduliwa.

Kama sehemu ya juhudi za kueneza lugha hiyo nchini, Bi Kadaga alisema maafisa wote wakuu serikalini, wakiwemo mawaziri na majaji, wanasoma masomo ya lazima kila wiki.

Mnamo Julai 2022, serikali ya Uganda iliidhinisha kupitishwa kwa Kiswahili kama lugha rasmi na kuagiza kuwa somo la lazima katika shule za msingi na upili.

Lakini lugha hiyo kwa sasa inafundishwa katika shule chache za sekondari nchini.

Takriban watu milioni 200 wanazungumza Kiswahili duniani na mwaka wa 2021, lugha hiyo ilipata msukumo mkubwa zaidi pale Umoja wa Mataifa ulipoteua tarehe 7 Julai kuwa Siku ya Lugha ya Kiswahili Duniani.

Pia ni lugha rasmi ya kanda ya Afrika Mashariki, EAC.

Mnamo 2019, Kiswahili kilikua lugha pekee ya Kiafrika kutambuliwa na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (Sadc).

Pia kuna juhudi za kuitambulisha katika madarasa kote Afrika Kusini na Botswana.

Chanzo: Bbc