Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali ya Uganda yafuta kesi dhidi ya mkosoaji mkubwa wa serikali

Uganda Picww Serikali ya Uganda yatupilia mbali kesi dhidi ya Mkosoaji mkubwa wa serikali

Tue, 14 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali ya Uganda imetupilia mbali kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Mwanasheria na Wakili nguli wa utetezi wa haki za binadamu, Nicholas Opiyo, mara baada ya kuibuka kwa vilio vya watu wengi wakihofia ukandamizwaji mkubwa unaofanywa dhidi ya asasi za kiraia nchini humo.

Mwanasheria huyo mpiganiaji wa haki, ni mkosoaji mkubwa wa Seriklai ya nchini humo inakumbukwa kuwa alikamatwa Desemba mwaka 2020, hatua ambayo ilionekana kama vita ya kisiasa hali iliyopelekea mamlaka za nchini humo kukosolewa vikali na wafatiliaji wa mienendo ya haki za binadamu duniani.

Nicholas alituhumiwa kwa makosa ya kuhujumu fedha za misaada zilizotolewa na shirika la misaada la Marekani kwa ajili ya kuwezesha shuguli za Asasi za Kiraia. Fedha hizo zilitajwa kuwa ni dola 340,000 sawa na shilingi Milioni 7.90 za kitanzania.

Kesi hii imefutwa mara baaada ya upande wa mashtaka kushindwa kutleta ushahidinakuamua kutupilia mbali madai hayo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live