Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali ya Rwanda yashutumu matamshi ya rais wa Burundi

Serikali Ya Rwanda Yashutumu Matamshi Ya Rais Wa Burundi Serikali ya Rwanda yashutumu matamshi ya rais wa Burundi

Tue, 23 Jan 2024 Chanzo: Bbc

Serikali ya Rwanda imeshtumu matamshi yaliotolewa na rais wa Burundi Evariste Ndayishimiyewakati wa hafla moja mjini Kinshasa wikendi iliopita.

Kulingana na taarifa ya serikali ya Rwanda iiochapishwa katika mtandao wa Twitter, matamshi hayo ‘yasio na msingi’ yalilenga kuchochea mgawanyiko nchini Rwanda kwa, kuzua ghasia na kuharibu amani katika eneo lote la maziwa makuu.

Taarifa hiyo kwa vyombo vya habari ilisema kwamba raia wa Rwanda walifanya bidi kuimarisha Umoja na maendeleo na kwamba kwa mtu yeyote kujaribu kuwataka vijana wa taifa hilo kupindua serikali yao inakera.

Iliongezea kwamba inakera zaidi kwa kiongozi Jirani kutoa matamshi kama hayo katika hafla ya Umoja wa Afrika suala ambalo ni ukiukaji wa mkataba wa AU.

Hatahivyo taarifa hiyo ilihitimisha kwamba taifa la Rwanda halina haja ya kuzua ghasia na majirani zake na kwamba litaendelea kushirikiana na majirani zake katika eneo hili na kwengineko kuimarisha udhibiti na maendeleo.

Katika mahojiano na vijana Jumapili mjini Kinshasa, Rais Ndayishimiye alikosoa mamlaka ya Rwanda kwa kusaidia "makundi yanayovuruga eneo hilo".

Ndayishimiye pia alisema kwamba "ni muhimu kuendeleza mapambano hadi watu wa Rwanda wenyewe waanze kutoa shinikizo", na kuongeza: "Nadhani hata vijana wa Rwanda hawawezi kukubali kuwa wafungwa katika eneo hilo".

Utawala wa Gitega umekuwa ukiitizama Kigali kwa jicho baya tangu mwishoni mwa mwaka jana walipoishutumu Rwanda kwa kusaidia kundi la RED-Tabara lililofanya shambulio baya kaskazini na magharibi mwa Burundi.

Serikali ya Rwanda ilisema haina uhusiano wowote na shambulio hilo. Serikali ya Burundi baadaye ilifunga mpaka wake na Rwanda.

Wataalamu wa Umoja wa Mataifa wanalishutumu jeshi la Burundi kwa kushirikiana kinyume na jeshi la DR Congo katika vita dhidi ya kundi la M23, wataalamu hao pia wanalishutumu jeshi la Rwanda kwa kusaidia M23.

Wakati pande zote mbili zikikanusha hilo, baadhi ya wachambuzi wanasema kuwa nafasi ya Gitega na Kigali katika vita mashariki mwa Congo huenda ikawa sababu mojawapo ya hali ya sasa kati ya Burundi na Rwanda.

Chanzo: Bbc