Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali ya Mali kujenga chuo cha kivita

Mali War College Serikali ya Mali kujenga chuo cha vita

Fri, 24 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baraza la Mpito la nchini Mali limepitisha muswaada wa sheria wa kuanzishwa kwa chuo maalum cha kivita wakati wa mkutano wa Bunge ambao pia ni la mpito.

Chuo hicho cha kivita kinatarajiwa kutoa mafunzo ya kiwango cha juu kwa maafisa wakuu wa vikosi vya ulinzi na usalama, Askari polisi pamoja na watendaji wengine wa raia, pia kitakuwa ni kituo cha utafiti juu ya mikakati ya ulinzi na usalama itakayo fanywa kwa kushirikiana na wasomi wa nchini humo.

Aidha, maafisa watako hitimu katika chuo hicho watapata nafasi za juu zaidi ndani ya jeshi la nchini humo pamoja na kupelekwa katika kazi maalumu za kimataifa kama zile za wajumbe wa kulinda amani wa UN.

Hata hivyo inaelezwa kuwa, ujenzi wa chuo hicho umekuwa ukizungumziwa kwa miaka kadhaa, hatua hii imepongezwa na baadhi ya viongozi wa mpito nchini humo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live