Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali ya Kenya yatafuta idhini ya kutumia Sh.Bilioni 10 kukabiliana na mafuriko

Serikali Ya Kenya Yatafuta Idhini Ya Kutumia Sh.Bilioni 10 Kukabiliana Na Mafuriko Serikali ya Kenya yatafuta idhini ya kutumia Sh.Bilioni 10 kukabiliana na mafuriko

Mon, 6 May 2024 Chanzo: Bbc

Bunge la taifa nchini Kenya kuidhinisha shilingi bilioni 10.6 kwa ajili ya kukabiliana na dharura ya mafuriko na misaada ya kibinadamu kwasababu ya mvua kubwa inayoendelea kunyesha kote nchini humo.

Maelezo ya fedha hizo yapo kwenye bajeti ya II ya ziada katika kipindi cha mwaka wa fedha mwaka 2023/2024.

Kufikia Jumamosi zaidi ya watu 228 walikuwa wamefariki dunia kutokana na mafuriko na maelfu ya watu kujeruhiwa huku wengine wengi wakilazima kuhama makazi yao.

Mvua hiyo isiyokoma imeharibu mazao na mali huku serikeli ikitenga makazi ya muda kwa watu waliohama makwao.

Hatua hii inafuatia tangazo ya mamlaka ya hali ya hewa la kunyesha kwa mvua kubwa katika maeneo mengi kote nchini humo.

Chanzo: Bbc