Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali ya Kenya yasitisha shughuli za Worldcoin ikitaja hofu za kiusalama

Serikali Ya Kenya Yasitisha Shughuli Za Worldcoin Ikitaja Hofu Za Kiusalama Serikali ya Kenya yasitisha shughuli za Worldcoin ikitaja hofu za kiusalama

Wed, 2 Aug 2023 Chanzo: Bbc

Serikali ya Kenya imesitisha shughuli zote zinazohusiana na mradi wa sarafu fiche za kidijitali wa WorldCoin.

Waziri wa Usalama wa Ndani nchimi humo Kithure Kindiki amesema kupitia taarifa kwamba serikali ina wasiwasi kuhusu mradi huo tata ambao kufikia sasa umesajili maelfu ya Wakenya, na kwamba marufuku hiyo itaendelea kutekelezwa hadi mashirika husika yatakapothibitisha kutokuwepo kwa hatari yoyote ya kiusalama .

“Vyombo husika vya usalama, huduma za kifedha na ulinzi wa data vimeanza uchunguzi ili kubaini ukweli na uhalali wa shughuli zilizotajwa hapo juu, usalama na ulinzi wa takwimu zinazokusanywa , na jinsi wahusika wanavyokusudia kutumia data,” imesema sehemu ya taarifa hiyo.

"Zaidi ya hayo, itakuwa muhimu kwamba uthibitisho wa usalama wa umma na uadilifu wa miamala ya kifedha inayohusisha idadi kubwa ya raia utolewe kwa njia ya kuridhisha mapema."

Kindiki aliongeza kuwa iwapo mtu yeyote atapatikana kusaidia au kujihusisha zaidi na shughuli hizo atachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.

Siku ya Jumanne, foleni ndefu zilishuhudiwa katika Jumba la (KICC) jijini Nairobi ambapo maelfu walimiminika kwa siku ya pili ili kujiandikisha kwa mradi huo, ambapo wanaruhusu kuchanganuliwa kwa data ya mboni zao za macho kwa tokeni maalum za sarafu za kidijitali zenye thamani ya shilingi 7,700

Maafisa waliiomba timu ya Worldcoin kusitisha zoezi hilo na kuwatimua watu hao kutokana na kile walichosema ni hatari za kiusalama.Waliambia timu hiyo itafute uwanja mkubwa zaidi kama vile viwanja vya Nyayo au Kasarani.

Kamishna wa Data Immaculate Kassait alisema tume hiyo inafanya tathmini yake kwa mchakato mzima wa Worldcoin ili kuhakikisha uzingatiaji wa sheria.

Mradi huo wa Mkurugenzi Mtendaji wa OpenAI Sam Altman umekosolewa vikali kuhusu masuala ya usiri na usalama wa data.

Chanzo: Bbc