Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali ya Kenya yachagua kikosi mazungumzo na upinzani

Serikali Ya Kenya Yachagua Kikosi Mazungumzo Na Upinzani Serikali ya Kenya yachagua kikosi mazungumzo na upinzani

Tue, 11 Apr 2023 Chanzo: Bbc

Wabunge wa muungano unaotawala nchini Kenya wamekutana leo na kuchagua timu ya kujadiliana na upinzani kuhusu gharama ya maisha na masuala mengine yaliyosababisha maandamano ya wiki kadhaa mwishoni mwa mwezi Machi.

Muungano huo wa Kenya Kwanza umechagua ujumbe wake wa watu saba kwenye mazungumzo ya wabunge wa pande mbili na upinzani.

Wakati wa mkutano na wanahabari katika Ikulu Jumanne, Kiongozi wa Wengi katika Bunge la Kitaifa Kimani Ichung'wa alisema kuwa wabunge hao walichaguliwa kufuatia majadiliano wakati wa mkutano wa awali wa Kikundi cha Wabunge wa Kenya Kwanza.

Kiongozi wa upinzani Raila Odinga mnamo tarehe 4 Aprili alitishia kuitisha maandamano mapya iwapo serikali itashindwa kuyachukulia kwa uzito mazungumzo hayo.

Upinzani ulikuwa umesitisha maandamano tarehe 2 Aprili baada ya Ruto kuitisha mazungumzo.

Muungano wa Azimio la Umoja wa Odinga- One Kenya umetaja timu ya watu saba kwa ajili ya majadiliano hayo.

Inaitaka serikali kuchukua hatua za kupunguza gharama ya maisha, kufanya mageuzi ya uchaguzi, kufungua seva za tume ya uchaguzi na kuacha kuajiri maafisa wa wakala wa kura.

Chanzo: Bbc