Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali ya Haiti inafanyia kazi mpango wa kuwapokea polisi wa Kenya

Mahakama Ya Kenya Yazuia Kutumwa Kwa Polisi Nchini Haiti Serikali ya Haiti inafanyia kazi mpango wa kuwapokea polisi wa Kenya

Thu, 15 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali ya Haiti, juma hili imesema inafanyia kazi makubaliano rasmi na nchi ya Kenya ili kuhakikisha polisi wake wanatumwa nchini humo, kwenda kuisaidia kukabiliana na makundi ya wahalifu.

Maafisa wa ngazi za juu kutoka nchi zote mbili walikutana nchini Marekani kwa siku tatu wiki hii, ili kuandaa mkataba wa maelewano na kuweka makataa ya kuwasili kwa vikosi vya Kenya.

Mikutano hiyo iliyofanyika faragha ilijumuisha maafisa wakuu wa Marekani na imefanyika wiki kadhaa baada ya mahakama nchini Kenya kuzuia kutumwa kwa polisi hao kwa kile ilisema hakukuwa na maombi wala makubaliano rasmi baina ya nchi hizo mbili na nikinyume cha sharia.

Haijabainika mara moja ni jinsi gani mkataba huu wa maelewano unaweza kukwepa uamuzi wa mahakama.

Mwaka 2022 waziri mkuu wa Haiti, Ariel Henry, aliomba usaidia kutoka Jumuiya ya kimataifa, ambapo kenya ilijitolea kuongoza kikosi maalumu kabla ya baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mwaka mmoja baadaye kuidhinisha mpango huo.

Haya yanajiri wakati huu watu zaidi ya mia nane wakiripotiwa kuuawa au kutekwa nyara nchini Haiti na makundi yenye silaha, tangu mwezi Januari mwaka huu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live