Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali kufanya uhakiki wa vyeti watumishi wa umma

3ad6e99638e3a5595907ffd03304c7d5 Serikali kufanya uhakiki wa vyeti watumishi wa umma

Tue, 10 Nov 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

WAZIRI wa Utumishi wa Umma, Bangasi Bakosoro amesema serikali itafanya ukaguzi wa vyeti kwa wafanyakazi wake.

Amesema hatua hiyo ni muhimu kuchukuliwa kutokana na kuwapo ongezeko la watu wanaotumia vyeti feki ili kupata ajira katika utumishi wa umma.

Akizungumza mjini hapa juzi, waziri huyo alisema watumishi watakaobainika kuwa na vyeti feki watafukuzwa kazi ili kuajiriwa wenye sifa.

“Tutafanya uhakiki katika faili za kila mfanyakazi. Tunafahamu kuwa hii itachukua muda mrefu lakini lazima ifanyike na tumeshaanza. Tunataka kuona kwamba wale ambao wana sifa ya kupata kazi wanapata kazi na wale wenye vyeti feki wanaachia nafasi hizi kwa wengine,” alisema.

Bakosoro alisema waombaji wengi wa kazi serikalini wamekutwa na vyeti feki kutoka Wizara ya Elimu na kwamba wanatarajia kufungua kesi dhidi ya wote waliobainika kufanya udanganyifu na kuwa sheria na taratibu zitawekwa kushughulikia masuala hayo.

“Tunawaonya walioajiriwa na serikali kwa kutumia vyeti feki vya elimu na tunawashauri wenye matokeo yasiridhisha kuongeza elimu ili kuwawezesha kupata fursa ya kupandishwa vyeo kwani kuna walioajiliwa na kiwano cha 1,12 na 10 ambao hawana shahada au diploma,” alisema.

Bakosoro alisma kwa kutumia teknolojia ya kisasa, serikali itafanya ukaguzi kwenye vyuo vikuu kuhakiki vyeti vya wafanyakazi wake na watakaobainika kufanya udanganyifu watachukuliwa hatua za kisheria.

Chanzo: habarileo.co.tz