Waziri wa mambo ya ndani (CS) Kithure Kindiki ametangaza kanisa la Good News International Ministries la muhubiri Paul Mackenzie kuwa kundi la uhalifu..
Katika taarifa yake aliyoitoa Jumatano, Kindiki alisema tamko hilo ni kwa mujibu wa Kifungu cha cha Sheria ya Kuzuia Uhalifu wa Kupangwa.
Kifungu kilichotajwa kinaeleza kwamba “Endapo Waziri ana sababu za msingi za kuamini kuwa kikundi fulani kinajihusisha na uhalifu wa kupangwa chini ya kifungu cha 3 cha Sheria hii, anaweza, kwa ushauri wa Kamishna wa Polisi, kwa notisi, kutangaza kwamba ni kundi la uhalifu uliopangwa kwa madhumuni ya Sheria hii.
"Pat (2) inasema kwamba "Mtu yeyote ambaye hakuridhika na uamuzi wa Waziri chini ya kifungu hiki anaweza kuomba Mahakama Kuu ili kusuluhishwa ndani ya siku ishirini na moja tangu tarehe ya kuchapishwa kwa amri."
Waziri huyo na maafisa wake yuko katika eneo la Shakahola, Kaunti ya Kilifi, eneo linalomiliki dhehebu linaloshukiwa kuhusika na vifo vya zaidi ya watu 400 vilivyotokea kati ya Januari 2021 na Septemba 2023.
Kesi za mahakama zinazomkabili Mchungaji Mackenize na washtakiwa wengine 94 zimebaini kuwa nyenzo za DNA kutoka miili 429 kwa ajili ya uchunguzi zimezuiwa kutokana na kuoza kwa miili 360, na kufanya zoezi la uchunguzi wa maiti kuwa gumu, lenye gharama kubwa, na lilichokuwa muda mrefu.
Washukiwa hao wanakabiliwa na mashtaka 238 yanayowakabili yakiwemo ugaidi na itikadi kali.
Wamekana mashtaka yote.Mackenzie na washtakiwa wenzake ambao wamekaa rumande kwa miezi kadhaa, wataendelea kusalia rumande kufuatia ombi la upande wa mashtaka la kutaka kuendelea kuwazuilia hadi kukamilika kwa upelelezi.
Mwishoni mwa Disemba, mahakama ya Shanzu ilikubali ombi la upande wa mashtaka la kuongeza muda wa kuzuiliwa kwa washukiwa kwa siku 180 zaidi.