Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali Congo shughuli zisizo za michezo kwenye viwanja baada yatu tisa kufariki

Serikali Congo Shughuli Zisizo Za Michezo Kwenye Viwanja Baada Yatu Tisa Kufariki.png Serikali Congo shughuli zisizo za michezo kwenye viwanja baada yatu tisa kufariki

Mon, 29 Jul 2024 Chanzo: Bbc

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imesitisha shughuli zote zisizo za michezo kwenye viwanja vya michezo vya 'stade des Martyrs' na 'stade Tata Raphaël', katika mji mkuu Kinshasa, baada ya takriban watu tisa kufariki katika 'stade des Martyrs' wakati wa tamasha la nyimbo za injili.

Wizara ya Mambo ya Ndani inasema wale waliofariki katika tamasha la Jumamosi la mwimbaji na mtunzi wa nyimbo za Injili Mike Kalambay walikufa kwa "kukosa hewa" kutokana na msongamano.

Watu wengine 19 pia walijeruhiwa katika tamasha hilo.

Mwimbaji Kalambay hakuwa ametangaza chochote hadharani.

'Stade des Martyrs' una uwezo wa kuchukua watu 80,000.

Huku 'Stade Tata Raphaël' ukiwa na uwezo wa kuwapokea watu 40,000.

Uwanja huu ni maarufu kwa kuwa ukumbi wa pambano la ndondi la Muhammad Ali dhidi ya George Foreman lilifanyika katika uwanja huo mnamo mwaka 1974.

Chanzo: Bbc