Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Seneti yaidhinisha Mswada wa BBI, maseneta 51 wasema "ndio"

0dbb23e0aab740f3 Seneti yaidhinisha Mswada wa BBI, maseneta 51 wasema "ndio"

Wed, 12 May 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

- Jumanne alasiri, maseneta 51 walipiga kura ya ndio kuidhinisha huo, huku maseneta 12 wakipiga kura dhidi yake

- Kura hiyo inajiri chini ya wiki moja baada ya Bunge la Kitaifa kupiga kura ya kuunga mkono Mswada huo, huku waungaji mkono wa mswada huo wakitazamia kura ya maamuzi mwezi Julai au Agosti

- Wakati huo huo, uamuzi wa ikiwa Kenya itafanya kura ya maamuzi kulingana na mapendekezo ya watetezi wa BBI sasa iko mikononi mwa majaji watano: Jaji Chacha Mwita, Joel Ngugi, George Odunga, Jarius Ngaah na Janet Mulwa

Mbunge la Seneti limepitisha mapendekezo ya marekebisho ya katiba kupitia Mswada wa BBI bila marekebisho.

Jumanne alasiri, maseneta 51 walipiga kura ya ndio kuidhinisha huo, huku maseneta 12 wakipiga kura dhidi yake.

Seneta Isaac Mwaura, ambaye alifukuzwa rasmi kutoka kwenye wadhifa wake aliopewa na Chama cha Jubilee kwa sababu za utovu wa nidhamu, hakushiriki zoezi hilo.

Kura hiyo inajiri chini ya wiki moja baada ya Bunge la Kitaifa kupiga kura ya kuunga mkono Mswada huo, huku waungaji mkono wa mswada huo wakitazamia kura ya maamuzi mwezi Julai au Agosti.

Spika wa Seneti anatarajiwa kupeleka uamuzi wa Maseneta kwa Rais Uhuru Kenyatta, kabla ya kupelekewaTume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC).

Wakati huo huo, uamuzi wa ikiwa Kenya itafanya kura ya maamuzi kulingana na mapendekezo ya watetezi wa BBI sasa iko mikononi mwa majaji watano: Jaji Chacha Mwita, Joel Ngugi, George Odunga, Jarius Ngaah na Janet Mulwa.

Wanye kesi ambao ni mchumi David Ndii, Umoja wa Kitaifa wa Wauguzi Kenya, Thirdway Alliance, 254Hope, Justus Juma na Moraa Omoke walilalamika kuhusu mchakato wa BBI kurekebisha Katiba wakisema ni hatua hatari.

Katika mawasilisho yaliyotolewa na mawakili wanaowakilisha vikundi 8, benchi la majaji watano lilihimizwa kutumia nguvu za korti zisizo na kikomo kuondoa majaribio ya kurekebisha Katiba

Mapema siku hiyo, Spika wa Seneti Kenneth Lusaka katika barua kwa maseneta, alisema kwamba Bunge - ambalo limepewa jukumu la kuwakilisha mapenzi ya watu - haliwezi kudai kwenda kinyume na mapenzi ya watu ambao wamejieleza wazi.

"Ni njia inayochukuliwa na raia wanaotambua kuwa mamlaka yote ya enzi ni mali ya watu wa Kenya, kama ilivyoelezwa katika Kifungu cha 1 cha Katiba, na kwamba watu wa Kenya wanaweza kutumia mamlaka yao ya kiutawala moja kwa moja au kupitia wawakilishi waliochaguliwa kidemokrasia," alisema.

Aliendelea: "Nina hakika kwamba ujenzi sahihi wa Katiba hutupeleka kwenye hitimisho kwamba mamlaka yaliyopewa dhamana ya Bunge ya kutekeleza enzi ya watu kwa kuwakilisha mapenzi yao hayawezi na haiwezi kupanua kupindua, kubadilisha au kubadilisha ile mapenzi na yake mwenyewe hekima, ambapo watu wamejieleza bila shaka. ”

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke