Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Seneta mbaroni kwa kulaghai wanafunzi

Jackson Mandago Jackson Mandago.

Thu, 17 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Seneta mmoja nchini Kenya amekamatwa kuhusiana na kashfa ya ulaghai kwenye mpango wa kupeleka wanafunzi kusoma nchini Finland na Canada.

Jackson Mandago na watu wengine watatu wanakabiliwa na makosa 11 ikiwemo wizi na matumizi mabaya ya ofisi.

Mandago anatuhumiwa kuhusika na kashfa ya kupotea kwa dola za Kimarekani milioni 7.6 zilizotakiwa kusomesha wanafunzi wakikenya nchini Finland na Canada.

Hivi sasa mamia ya wanafunzi waliokwishalipia mpango huo wa elimu wamekwama nchini Kenya.

Wanafunzi waliofanikiwa kuondoka wamejikuta hawana pa kuishi na hata kuanza kurudishwa Kenya baada ya kaunti ya Uasin Gishu kushindwa kutuma pesa za malazi na ada.

Ulaghai huu ulitokea wakati Bw.Mandago alipokuwa Gavana.

Rais William Ruto ametaka uchunguzi wa kina ufanyike juu ya kashfa hiyo na ameamuru wahusika kuzilipa pesa hizo haraka.

Aidha Ruto ameahidi kuwa baada ya matokeo ya uchunguzi huo walioathirika watapatiwa ufadhili wa masomo nchini Kenya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: