Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Seneta afurahia Odinga kuondolewa AU

Seneta Afurahia Odinga Kuondolewa AU Seneta afurahia Odinga kuondolewa AU

Thu, 23 Feb 2023 Chanzo: Radio Jambo

Seneta wa kaunti ya Nandi Samson Arap Cherargei mnamo tarehe 23 Februari alijibu uamuzi wa Muungano wa Afrika wa kusitisha muda wa Raila Odinga kama mwakilishi wake mkuu.

Akizungumza kupitia ukurasa wake rasmi wa twitter, Seneta Samson Arap Cherargei alifichua kuwa ni mara ya kwanza waziri mkuu wa zamani Raila Odinga kukubali uamuzi.

Cherargei ambaye ni mshirika wa Ruto vilevile alitoa maoni yake kuwashukuru Umoja wa Afrika kwa kumfuta kazi Bw Odinga kama mwakilishi wao mkuu kwa miundo msingi na maendeleo.

Alifafanua kauli yake kwa kudai kuwa anastahili kufutwa kazi kwa kuendelea kuhujumu serikali halali inayoongozwa na rais William Ruto na naibu wake Rigathi Gachagua.

Cherargei pia alidai kuwa waziri mkuu wa zamani Raila Odinga anafaa pia kuweka lami kama Wakenya wa kawaida na pia hatapata muda zaidi hatua yake kubwa dhidi ya serikali ya Kenya Kwanza.

"Tinga kwa mara ya kwanza katika maisha yake amekubali uamuzi. Asante AU kwa kumtimua Tinga kwa kuendelea kuhujumu serikali halali ya Kenya inayoongozwa na Mh Ruto. Tinga pia anapaswa kuhangaika kama mkenya mwingine yeyote na pia muda zaidi wa maandamano yake. !Kimeumana !"

Maoni yake yanajiri baada ya Raila Odinga kuvunja ukimya akishukuru Umoja wa Afrika kwa nafasi nzuri waliyompa kama mjumbe wa Muungano.

Inavyoonekana, kutimuliwa kwa Bw Odinga kumezua hisia tofauti kutoka kwa wakenya pamoja na viongozi wengine.

Katika tangazo lililotolewa na Mwenyekiti wa Tume ya Muungano wa Afrika, Moussa Faki Mahamat, muungano huo ulimtakia Bw Odinga mema na kutumaini kuwa bado atakuwa wa thamani kwa muungano huo.

"Jukumu lako katika safari hii, Mheshimiwa, limekuwa muhimu sana. Niruhusu nitoe shukrani zangu za dhati kwa kukubali kuhudumu katika jukumu hili wakati wa kipindi cha mpito, ambacho sasa kimefikia tamati ya furaha,” Bw Faki alisema.

Bw Odinga aliteuliwa kuwa Mwakilishi Mkuu wa Miundombinu barani Afrika mnamo Oktoba 20, 2018, wakati wa uongozi wa Rais mstaafu Uhuru Kenyatta.

Uteuzi wake ulikuwa uamuzi wa msukumo wa Umoja wa Afrika wa kuharakisha ushirikiano wa bara hilo kupitia miundombinu, ili kukuza ukuaji wa uchumi na maendeleo endelevu.

Chanzo: Radio Jambo