Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Seneta Mutula Kilonzo atangaza siku ambayo Rais atazuru eneo la Ukambani

6ff0905c0942604c Seneta Mutula Kilonzo atangaza siku ambayo Rais atazuru eneo la Ukambani

Wed, 7 Jul 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Ziara ya rais Uhuru Kenyatta maeneo ya Ukambani iliahirishwa kwa ajili ya ongezeko la virusi vya COVID-19Kulingana na ripoti kutoka kwa ofisi ya Rais, ilihofiwa kwamba maambukizi mapya ya virusi hivyo yangeripotiwaRais alikuwa amepanga kuzuru kaunti za Machakos na Makueni siku ya Jumanne, Julai 6 kabla ya kuzuru kaunti zingine Ziara ya Rais Uhuru Kenyatta iliyoratibiwa kuanza siku ya Jumanne, Julai 6 eneo la Ukambani iliahirishwa kwa ajili ya ongezeko la maambukizi ya virusi vya covid- 19.

Akizungumza kwenye mahojiano na KTN News, Seneta wa Makueni Mutula Kilonzo aliwahakikishia wakazi kwamba Rais bado atazuru maeneo hayo lakini sio siku uliyokuwa umepangwa.

"Msambao wa virusi vya COVID- 19 ndio wasi wasi mkubwa na ndio sababu Rais hajaweza kuzuru maeneno haya, alikuwa awahutubie wakazi wa Ukambani lakini lazima masharti ya covid-19 yazingatiwe," Mutula alsema.

Hata hivyo, viongozi wametakiwa kujipanga na waelewane ni maendeleo yapi Rais atatatakiwa kufanya maeneo hayo atakapozuru.

" Tumeahirisha ziara ya rais na tunatarajia azuru Julai 29 lakini bado tutakuwa na mkutano na Rais Uhuru Kenyatta wiki hili," Mutula alisema.

Wakati huo huo, Kilonzo alifutilia mbali madai kwamba viongozi kutoka Ukambani wametofautiana kisiasa na ndio sababu Rais amekataa kufika eneo hilo.

" Tuna miradi mingi ambayo kila kiongozi kutoka Ukambani anataka kuonyesha na siku mbili kwa ziara ya rais haitoshi," Mutula alisema.

Kulikuwa na uvumi kwamba viongozi kutoka chama cha Kalonzo Musyoka na baadhi ya viongozi kutoka eneo hilo walikuwa wametofautiana kuhusu ziara ya rais, madai ambayo bado haijadhibitishwa.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Tazama Video Kemkem za Kusisimua Kutoka hapa TUKO.co.ke

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke