Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Senegal yawaachia mamia ya wafungwa wa kisiasa

Senegal Yawaachia Mamia Ya Wafungwa Wa Kisiasa Senegal yawaachia mamia ya wafungwa wa kisiasa

Wed, 21 Feb 2024 Chanzo: Bbc

Waziri wa Sheria wa Senegal Aissata Tall Sall ametangaza kuachiwa huru kwa karibu waandamanaji 400 kutoka gerezani.

Walikamatwa na kufungwa wakati wa maandamano ya kisiasa ya Machi 2021 na Juni 2023.

Bi Sall hakusema ikiwa kiongozi wa upinzani Ousmane Sonko na mgombeaji urais Bachirou Diomaye Faye wataachiliwa.

"Kitu pekee ninachoweza kusema ni kwamba hii sio kutolewa kwa wingi; hizi ni kesi ambazo zinasomwa kwa msingi wa makosa kulingana na vipengee kwenye faili," aliongeza.

Waziri huyo alisema kuachiwa kwa wafungwa hao wa kisiasa kunalenga kupunguza hali ya wasiwasi nchini.

Maandamano ya kisiasa nchini Senegal mara nyingi yamesababisha vurugu na vifo.

Hivi majuzi, watu watatu walikufa wakati wa maandamano ya kufutwa kwa uchaguzi wa Februari 25 nchini humo.

Waziri wa sheria alisema uchunguzi unaendelea ili kubaini waliohusika.

Chanzo: Bbc