Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Senegal yataka Israel itengwe

Netanyahu Asema Israel Inaweza 'kujitegemea' Ikiwa Marekani Itasita Kuipa Silaha Senegal yataka Israel itengwe

Mon, 2 Sep 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri Mkuu wa Senegal, Ousmane Sonko ameziasa nchi za Kiislamu kuususia utawala wa Israel na kuzidisha mashinikizo ya kulitenga dola hilo la Kizayuni.

Sonko amesema hayo wakati akishiriki maandamano mapya ya Wasenegal ya kuwaunga mkono wananchi wa Palestina wanaotaabika kutokana na athari za vita katika Ukanda wa Gaza.

Kiongozi huyo wa Senegal amemtaja Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu kama mtu anayefadhilisha kuponda maelfu ya miili chini ya miguu yake ili kuepuka kukabiliwa na mkono wa sheria.

Sonko ametoa wito wa kuwepo mshikamano zaidi miongoni mwa nchi za Kiislamu ili kuiunga mkono Palestina na kusisitiza kuwa, "Lazima tuwalete pamoja wale wote wanaochukizwa na dhulma hii, tufanye kazi kuelekea suluhisho la kisiasa ambalo ni suluhisho la kulitenga dola la Israel."

Waziri Mkuu wa Senegal amesema maandamano hayo yanashinikiza kukomeshwa ukatili ulioidhinishwa na baadhi ya nchi za Magharibi dhidi ya Wapalestina na kuongeza kuwa, "kulaani pekee hakutoshi; Senegal imedhamiria kuchukua hatua madhubuti zaidi."

Wananchi wa Senegal wamekuwa wakiandamana mara kwa mara wakitoa wito kwa seriikali yao kukata uhusiano wa kidiplomasia na utawala haramu wa Israel.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live