Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Senegal: Wapinzani waunda muungano kupinga muhula wa 3 kwa Rais Macky

Senegal: Wapinzani Waunda Muungano Kupinga Muhula Wa 3 Kwa Rais Macky Senegal: Wapinzani waunda muungano kupinga muhula wa 3 kwa Rais Macky

Mon, 17 Apr 2023 Chanzo: Voa

Zaidi ya vyama vya siasa 100 na makundi ya kiraia nchini Senegal Jumapili waliunda muungano kupinga muhula wa tatu kwa Rais Macky Sall.

Miezi 10 kabla ya uchaguzi wa rais, muungano huo katika tangazo lake umetoa wito kwa Sall kuheshimu katiba na kujizuia kuwania tena uongozi kwa muhula wa tatu kwani ni “kinyume cha sheria na siyo halali.”

Rais huyo ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka 2012, hajaeleza wazi nia yake lakini anatupilia mbali madai kwamba itakuwa kinyume cha katiba kwake kugombea tena.

Mpinzani wake mkuu wa kisiasa, Ousmane Sonko alikuwa miongoni mwa viongozi kadhaa wa upinzani kushiriki kuanzishwa kwa muungano huo.

Zaidi ya vyama 120 Jumapili vilisaini mkataba wa vuguvugu liitwalo F24 Movement of Vital Forces, kulingana na waanzilishi wa vuguvugu hilo.

Muungano huo umetoa pia wito wa kuachiliwa kwa wafungwa wa kisiasa waliokamatwa wakati wa maandamano kuhusu kesi ya kashfa dhidi ya Sonko iliyowasilishwa na waziri wa utali Mame Mbaye Niang, mwanachama wa chama cha rais Sall.

Mvutano umeongezeka nchini humo kwa wiki kadhaa, huku maandamano yakivuruga shughuli katika mji mkuu Dakar.

Chanzo: Voa