Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Senegal: Wapinzani kadhaa waliachiliwa huru

SENEGAL Wapinzaniiii.png Senegal: Wapinzani kadhaa waliachiliwa huru

Fri, 16 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wapinzani kadhaa wameachiliwa huru siku ya Alhamisi nchini Senegal, inayokabiliwa na mgogoro tangu kutangazwa kuahirishwa kwa uchaguzi wa urais, kulingana na shirika la habari la AFP likinukuuu mawakili wawili na mwanachama wa Muungano wa Familia za Wafungwa.

"Wateja wangu wengi katika kesi zilizowekwa kwa ajili ya masuala ya kisiasa wanaachiliwa," Wakili Cheikh Koureissy Bâ ameliambia shirika la habari la AFP. Amehakikisha kuwa hii inawahusu wafungwa kadhaa. Katika orodha ya baadhi yao iliyotolewa kwa shirika la habari la AFP na Wakili Moussa Sarr ni pamoja na Alious Sané, mratibu wa vuguvugu la kiraia "Y'en a marre", Djamil Sane, meya wa wilaya ya Dakar na wanachama kadhaa wa chama cha upinzani cha zamani cha PASTEF, cha kiongozi wa upinzani, Ousmane Sonko.

Ishara ya kupunguza uhasama iliyotolewa na mamlaka ilitarajiwa baada ya kuhamasishwa kwa raia na upinzani dhidi ya kuahirishwa kwa uchaguzi wa urais na wito kutoka kwa washirika muhimu wa kimataifa wa Senegal kuandaa uchaguzi haraka iwezekanavyo. Watu watatu waliuawa katika maandamano yaliyopigwa marufuku na kukandamizwa na vikosi vya usalama wakati wa uhamasishaji huu.

"Shinikizo la kimataifa linasababisha Rais Macky Sall kuagiza kuachiliwa huru kwa wafungwa wa kisiasa," amesema Souleymane Djim, mwanachama wa Muungano wa Familia za Wafungwa wa Kisiasa, ambaye pia anathibitisha kuwa zoezi hili la watu kuachiliwa linaendelea.

Mmoja wa wagombea wakuu waliotangazwa kwa uchaguzi wa urais wa 2024, Ousmane Sonko, lakini pia wa naibu wake kama mkuu wa chama kilichofutwa cha PASTEF, Bassirou Diomaye Faye, wanazuiliwa tangu mwaka 2023. Kwa sasa hakuna habari juu ya uwezekano wao kuachiliwa.

Mamia kadhaa ya wanachama wa upinzani, zaidi ya elfu moja kulingana na baaadhi ya mashirika ya haki za binadamu, wamekamatwa tangu mwaka 2021 na mzozo wa madaraka kati ya Bw. Sonko, aliyehusishwa katika kesi kadhaa za kisheria, na rais Sall.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live