Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Senegal: Wakili wa Ousmane Sonko asema "hatujashindwa vita"

Polisi Wazingira Nyumba Ya Ousmane Sonko Wa Senegal Senegal: Wakili wa Ousmane Sonko asema "hatujashindwa vita"

Sun, 19 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakili wa mpinzani mkuu wa serikali ya Senegal amesema kuwa, uamuzi uliotolewa na Mahakama Kuu ya nchi hiyo hauna maana ya kushindwa vita katika jitihada za kinara wa upinzani, Ousmane Sonko za kugombea tena kiti cha rais katika uchaguzi ujao.

Babacar Ndiaye, mmoja wa mawakili wa Bw. Sonko, ameliambia shirika ya habari la AFP kwamba: "Uamuzi huu hautufai. Kesi itasikizwa tena, lakini mchakato wa ufadhili utakamilika hivi karibuni."

Kupata ufadhili ni hatua muhimu katika mchakato wa kugombea urais, ambayo lazima ifanyike kabla ya kuwasilisha maombi kuanzia Desemba 11 hadi 26.

Mahakama ya Kuu ya Senegal imebatilisha hukumu ambayo ingelimrejesha kiongozi wa upinzani, Ousmane Sonko, katika kinyang'anyiro cha urais mwezi Februari 2024, ikibainisha kuwa kesi hiyo itasikilizwa tena.

Rais wa mahakama hiyo amebatilisha na kufuta uamuzi wa mahakama ya Ziguinchor wa Oktoba 12 ambao uliamuru kusajiliwa upya kwa kiongozi wa upinzani, Ousmane Sonko, kwenye orodha za wapiga kura na hivyo kumruhusu kuwa mgombea urais.

Mahakama Kuu ya Senegal pia imerudisha kesi hiyo katika mahakama ya Dakar kwa ajili ya kusikilizwa upya kuhusu undani wa kesi yenyewe. Jaji wa Mahakama Kuu ya Senegal amesema, mahakama ya Ziguinchor ilitafsiri vingine kasoro ya utaratibu wa uchaguzi.

Mmoja wa mawakili wa Ousmane Sonko amesema Serikali inacheza mchezo wa paka na panya, na kwamba anasikitishwa sana na uamuzi huu, ambao amesisitiza kuwa utawanyima Wasenegali uchaguzi ambao ungemshirikisha mtu maarufu zaidi wa kambi ya upinzani.

Macky Sall Sonko, 49, ambaye katika uchaguzi wa rais wa 2019 aliibuka mshindi wa tatu, anamshtumu Rais Macky Sall wa Senegal, kwamba anafanya njama za kumzuia asishiriki tena kwenye uchaguzi wa rais.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live