Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Senegal: Wagombea kutunishiana misuli kampeni za mwisho

Rais Wa Senegal Asema Ataondoka Madarakani Tarehe 2 Mwezi Aprili Senegal: Wagombea kutunishiana misuli kampeni za mwisho

Fri, 22 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wagombea urais nchini Senegal wanafanya kampeni zao za mwisho leo Ijumaa kabla ya kupiga kura siku ya Jumapili, Machi 24, 2024 baada ya kampeni ya wazi lakini ya amani ikilinganishwa na miezi ya mvutano iliyotangulia uchaguzi huuwa kipekee.

Amadou Ba na Bassirou Diomaye Faye hasa, wanaochukuliwa kuwa washindani wawili wakuu katika uchaguzi ulio wazi zaidi katika historia ya Senegali huru, watajitokea leo kila mmoja akijaribu kuonyesha nguvu zake na kunadi sera zake kabla ya mwisho wa kampeni siku ya Ijumaa saa sita usiku saa za ndani. Propaganda zote zitapigwa marufuku.

Kambi ya mgombea wa upinzani Bassirou Diomaye Faye, aliyeachiliwa kutoka gerezani wiki moja iliyopita katikati ya kampeni, imepanga mkutano wa hadhara katika uwanja wa soka saa kumi alaasiri saa za ndani huko Mbour (magharibi). Kambi ya Amadou Ba, Waziri Mkuu wiki chache zilizopita na kuteuliwa na Macky Sall anayemaliza muda wake, imebaini kwamba itafanya kampeni yake ya mwisho huko Dakar na vitongoji vyake.

Zaidi ya Wasenegal milioni saba wameitwa Jumapili kumchagua rais wao wa tano katika kura ambayo haijaamuliwa kabisa, na ya kipekee katika mambo mengi. Kwa mara ya kwanza, kiongozi anayeondoka, aliyeongoza kwa miaka 12 na kuchaguliwa tena mwaka wa 2019, hatawania tena katika uchaguzi huo. Hapo awali Wasenegal walitakiwa kupiga kura mnamo Februari 25, lakini kuahirishwa kwa dakika za mwisho kulisababisha machafuko na vurugu za wiki kadhaa.

Kampeni ilifupishwa kutoka wiki tatu hadi mbili. Wanaume kumi na wanane na mwanamke mmoja, ambao wawili kati yao walitangaza kujiondoa mwishoni na kumuunga mkono Bw. Faye, walizunguka nchi nzima kwa dharura katika kuokoa muda kwa kunadi na kuwataka wafuasi wao kuwashawishi raia kumchagua kiongozi wao Bassirou Diomaye Faye. Changamoto ya tatu...

Wagombea hao walikaa kwa siku nyingi bila kula wala kunywa kutokana na kuahirishwa kwa uchaguzi huo na kufanyika katikati ya mwezi wa mfungo wa Waislamu. Amadou Ba na Bassirou Diomaye Faye wanapewa nafasi kubwa, mmoja wao kushinda uchaguzi huo. Tume ya uchaguzi imepiga marufu kutangaza au kuchapisha matokeo ya uchaguzi. Kuna uwezekano kufanyike duru ya pili, ambayo tarehe haijatangazwa.

Uchaguzi huo unafuatiliwa kwa karibu zaidi nje ya nchi kuliko ingekuwa katika nchi nyingine zinazoendelea. Ikiwa na wakazi milioni 18, Senegal ni mojawapo ya nchi tulivu zaidi katika Afrika Magharibi iliyotikiswa na mapinduzi ya kijeshi. Imedumisha uhusiano thabiti na nchi za Magharibi huku Urusi ikipanua ushawishi wake miongoni mwa majirani zake.Senegal inaweza kuanza kuzalisha mafuta na gesi mwaka huu.

Hata hivyo, Senegal imekumbwa na vipindi tofauti vya machafuko tangu mwaka 2021. Makumi ya watu waliuawa na mamia kukamatwa, na kuharibu taswira ya nchi, isivyo haki kulingana na serikali.

Idadi kamili ya kura zilizopigwa inahitajika ili kutangazwa kwa mshindi katika duru ya kwanza. Wasipofanya hivyo, wagombea wawili wakuu watashiriki duru ya pili. Matokeo ya muda yanaweza kujulikana mapema Jumapili usiku.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live