Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Senegal: Wagombea 70 wawasilisha fomu uchaguzi wa urais

Senegal Wagombea.png Senegal: Wagombea 70 wawasilisha fomu uchaguzi wa urais

Wed, 27 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Muda wa mwisho wa kuwasilisha fomu za wagombea katika uchaguzi wa urais nchini Senegal umekamilika Jumatano Desemba 27 saa sita usiku. Jumanne jioni, Desemba 26, wagombea 70 yaliwasilishwa fomu zao za uchaguzi kwa Baraza la Katiba.

Viongozi wa upinzani, pamoja na mgombea wa muungano tawala, wote wako katika orodha ya awali ya wagombea ambao watateuliwa rasmi Januari 4, 2024.

Ni mwezi wa Januari ambapo orodha ya wagombea ambao wataweza kuwania kiti cha urais itajulikana, wakati wa uchaguzi wa Februari 25, 2024. Wagombea 70 kwenye kiti cha urais, kwa sasa, watasubiri siku chache zaidi ambapo faili zao zitathibitishwa au la na Baraza la Katiba.

Miongoni wagombea hao ni pamoja na Amadou Ba, Waziri Mkuu wa Senegal na mgombea wa muungano unaotawala. Wengine kadhaa wamewasilisha faili zao kwa karani wa baraza hilo. Miongoni mwa wapinzani ni Ousmane Sonko, Khalifa Sall, Karim Wade, Idrissa Seck na hata magwiji wa siasa kama Abdoulaye Sylla na Rose Wardini.

Wote wanasubiri droo ambayo itafanywa Alhamisi Desemba 28 ili kubaini utaratibu wa uhakiki wa faili za udhamini na timu za Baraza la Katiba. Ni baada ya hatua hii tu ambapo kila ombi litatangazwa kuwa linakubalika au la.

Wagombea kadhaa walichagua ufadhili wa wabunge, wakiwa na wajibu wa kukusanya wabunge 13, ili kuepuka marudio katika orodha za udhamini. Nakala hizi zilikuwa sababu ya kutoshiriki kwa wagombea kadhaa katika uchaguzi wa urais wa mwaka 2019, ambapo wagombea watano pekee ndio walioidhinishwa.

Idadi hii inapaswa kuzidi kwa kiasi kikubwa katika uchaguzi ujao wa urais, kulingana na mmmoja wa waangalizi. Rais anayemaliza muda wake, Macky Sall, hatashiriki uchaguzi huo, kwa mara ya kwanza nchini Senegal.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live