Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Senegal: Wafungwa 400 wa kisiasa wameachiwa huru

Wafungwa Senegal.png Senegal: Wafungwa 400 wa kisiasa wameachiwa huru

Wed, 21 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa masuala ya haki nchini Senegal Aissata Tall Sall ametangaza kuachiwa huru kwa karibia waandamanaji 400 wa kisiasa kutoka jela.

Waandamanaji hao walikamatwa na kufungwa gerezani wakati wa maandamano ya mwezi Machi mwaka wa 2021 na mwezi Juni 2023.

Licha ya tangazo hilo, waziri Sall hakuweka wazi iwapo mwanasiasa wa upinzani Ousmane Sonko pamoja na mgombea wa urais Bachirou Diomaye Faye wataachiwa huru.

Aidha waziri huyo ameeleza kuwa hatua hiyo ya kuwaachia huru kwa wafungwa hao wa kisiasa imelenga kupunguza joto la kisiasa kwenye taifa hilo.

Maandamano ya kisiasa nchini Senegal yamekuwa yakifuatiwa na ripoti za watu kukamatwa na polisi, vifo pia vikithibitishwa kutokea.

Hivi karibuni, watu watatu walithibitishwa kufariki wakati wa maandamano ya kupinga kuhairishwa kwa uchaguzi mkuu wa tarehe 25 ya mwezi Februari.

Baada ya tangazo hilo, kiongozi huyo amesema uchunguzi unaendelea kubaini waliokuwa nyuma ya maandamano ya vurugu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live