Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Senegal: Waandamanaji wapinga uchaguzi kufanyika Juni

Uchaguzi Rais Senegal Senegal: Waandamanaji wapinga uchaguzi kufanyika Juni

Mon, 4 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mamia ya Waandamaji wameripotiwa kuendelea na maandamano ya kumshinikiza Rais Macky Sall kufanya Uchaguzi Mkuu ndani ya mwezi mmoja kabla ya muda wa Urais wake kumalizika April 2, 2024

Maandamano hayo yameendelea kwa zaidi ya mwezi mmoja ikiwa ni tangu Rais Sall atangaze kuahirisha Uchaguzi Mkuu uliopangwa kufanyika Februari 25, 2025 na badala yake kusogeza mbele hadi Desemba 15, 2024, muda ambao ulibatilishwa na Baraza la Katiba

Baadhi ya madai ya Waandamanaji ni pamoja na kuachiwa kwa Kiongozi wa Upinzani Ousmane Sonko. Wiki iliyopita, Rais Sall aliunda kikosi cha Maridhiano ambacho kilipendekeza Uchaguzi ufanyike June 2024, hata hivyo Upinzani umegomea pendekezo hilo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live