Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Senegal: Vurugu zaenea baada kuahirishwa kwa uchaguzi mpaka mwezi Desemba

Senegal: Vurugu Zaenea Baada Kuahirishwa Kwa Uchaguzi Mpaka Mwezi Desemba Senegal: Vurugu zaenea baada kuahirishwa kwa uchaguzi mpaka mwezi Desemba

Sat, 10 Feb 2024 Chanzo: Bbc

Maandamano makali nchini Senegal ya kupinga kuahirishwa kwa uchaguzi wa rais yameenea kote nchini, huku mauaji ya kwanza yakiripotiwa.

Mwanafunzi alifariki katika makabiliano na polisi siku ya Ijumaa katika mji wa kaskazini wa Saint-Louis, kiongozi wa upinzani na chanzo cha hospitali ya eneo hilo kilisema.

Katika mji mkuu Dakar, vikosi vya usalama vilifyatua gesi ya kutoa machozi na maguruneti kuwatawanya watu hao.

Uchaguzi wa Februari 25, umeahirishwa na wabunge hadi Desemba 15. Rais Macky Sall hapo awali alikuwa amesitisha uchaguzi huo kwa muda usiojulikana, akisema hili lilihitajika ili kutatua mzozo kuhusu stahiki kwa wagombea urais.

Wabunge baadaye waliongeza muda wa Bw.Sall kwa miezi 10.

Kiongozi wa upinzani Khalifa Sall, ambaye hana uhusiano na rais, awali alitaja kucheleweshwa kwa uchaguzi kuwa "mapinduzi ya kikatiba". Kifo cha mwanafunzi huyo huko Saint-Louis kiliripotiwa na Khalifa Sall katika chapisho kwenye mtandao wa kijamii.

"Mioyo ya wanademokrasia wote ilivuja damu kutokana na mlipuko huu wa mapigano yaliyochochewa na kusitishwa kwa mchakato wa uchaguzi bila sababu," alisema.

Kifo hicho kilithibitishwa na chanzo cha hospitali ya eneo kikizungumza kwa sharti la kutotajwa jina, na afisa katika chuo kikuu anachosoma mwanafunzi huyo, kulingana na shirika la habari la AFP.

Mamlaka ya Senegal haijazungumza lolote kuhusu suala hilo.

Chanzo: Bbc