Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Senegal: Viongozi wa upinzani Dias, Sonko na Gakou wakamatwa na polisi

Barthelemy DIAS Senegal: Viongozi wa upinzani Dias, Sonko na Gakou wakamatwa na polisi

Thu, 11 Nov 2021 Chanzo: SENEWS

Nchini Senegal, viongozi wa upinzani Barthélémy Dias, meya wa wilaya ya Mermoz Sacré Coeur, Malick Gakou, kiongozi wa chama cha "Grand Parti", na Ousmane Sonko, kiongozi wa chama cha PASTEF, wamepelekwa kwenye gari la polisi hadi katika kambi ya polisi ya Abdou Diassé leo Jumatano.

Barthélémy Dias aliitwa Jumatano hii asubuhi kwenye Mahakama ya Rufaa katika kesi ya mauaji iliyoanza mwaka wa 2011. Kesi hiyo iliahirishwa hadi Desemba 1 bila yeye kuwepo. Wakati huo huo, safari ya msafara wake kutoka nyumbani kwake huko Sicap Baobab ilikumbwa na matukio kadfhaa kati ya wafuasi na vikosi vya usalama, huku polisi ikilazimika kurusha mabomu ya machozi.

Baada ya saa kadhaa, Barthélémy Dias, lakini pia Malick Gakou na Ousmane Sonko - ambao walikuwa wakiandamana naye waliwekwa katika gari karibu na chuo kikuu. Walipelekwa katika kambi ya polisi ya Abdou Diassé.

Meya wa zamani wa Dakar Khalifa Sall, mmoja wa viongozi wa muungano wa upinzani wa Yewi Askan Wi (Waachilie huru kwa lugha ya Wolof), ana matumaini kwamba wenzi wake wataachiliwa hivi karibuni. Yeye haamini kuwa hii ni kesi.

Bado hakujatolewa maelezo kuhusu kwa nini watu hao watatu walichukuliwa na kupelekwa katika kambi ya polisi.

Chanzo: SENEWS