Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Senegal: Utata afya ya mwanasiasa aliyesusa kula kisa matokeo ya Urais

Senegal Upinzani Kula Tena Senegal: Utata afya ya mwanasiasa aliyesusa kula kisa matokeo ya Urais

Sat, 28 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nchini Senegal, barua kutoka kwa mkurugenzi wa mamlaka ya magereza aliyomuandikia Waziri wa Sheria kuhusu afya ya kiongozi wa upinzani Ousmane Sonko, ambaye alianza mgomo mpya wa kula mnamo Oktoba 17 dhidi ya kuzuiliwa kwake, inasambazwa kwenye mitandao ya kijamii.

Mwendesha mashtaka wa umma ametangaza kufunguliwa kwa uchunguzi ili kubaini chanzo cha uvujaji wa barua hii ambapo hali ya kiongozi wa chama cha PASTEF inaelezwa kuwa inahitaji "kuhifadhiwa katika uangalizi mkubwa".

Suala la kimatibabu kuhusu afya ya kiongozi wa upinzani nchini Senegal, Ousmane Sonko, linaendelea kuzua taharuki, baada ya kuvuja Oktoba 26, 2023 kwa barua ya mkurugenzi wa mamlaka ya magereza aliomwandikia Waziri wa Sheria ambayo inaonya juu ya hali ya afya ya kiongozi huyo wa chama cha PASTEF.

Majibu hayakuchukua muda mrefu: mwendesha mashtaka wa umma ametangaza kufunguliwa kwa uchunguzi ili kubaini chanzo cha uvujaji huu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live