Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Senegal: Serikali yapiga stop maandamano ya wapinzani

Senegal: Vurugu Zaenea Baada Kuahirishwa Kwa Uchaguzi Mpaka Mwezi Desemba Senegal: Serikali yapiga stop maandamano ya wapinzani

Tue, 13 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Maandamano yaliyokuwa yamepangwa kufanyika leo huko Senegal kupinga hatua ya Rais Macky Sall wa nchi hiyo ya kuakhirisha uchaguzi wa rais, yameakhirishwa baada ya serikali kuyapiga marufuku.

Uchaguzi wa Rais wa Senegal awali ulipangwa kufanyika mwezi huu wa Februari; hata hivyo umeakhirishwa na sasa utafanyika mwezi Disemba. Elymane Haby Kae mmoja wa waandaaji wa maandamano hayo amesema kuwa amepokea barua rasmi kutoka mamlaka husika kwamba maandamano ya kupinga kuakhirishwa uchaguzi wa rais yamepigwa marufuku kwa sababu yangetatiza pakubwa usafiri na kusababisha msongamano wa magari barabarani.

Naye Malick Diop, mratibu wa muungano ulioitisha maandamano hayo amesema kuwa wataakhirisha maandamano kwa sababu wanataka kuheshimu sheria. Wakati huo huo Wizara ya Mawasiliano, Huduma ya Simu na Nishati ya Kidijitali ya Senegal imesema kuwa wizara hiyo leo imesimamisha data ya simu za mkononi kutokana na kuenezwa jumbe kadhaa za chuki za uasi kwenye mitandao ya kijamii ambazo tayari zimechochea vurugu.

Uamuzi wa Rais Sall wa kuakhirisha uchaguzi wa rais ambao awali ulipangwa kufanyika tarehe 25 mwezi huu wa Februari, uliitumbukiza Senegal katika mgogoro na machafuko ya kisiasa, na watu watatu wameuawa kufuatia mapigano yaliyoibuka kati ya waandamanaji na polisi huko Dakar mji mkuu wa Senegal. Rais Macky Sall wa Senegal

Wapinzani nchini Senegal wamelaani vikali uamuzi wa Bunge kuahirisha uchaguzi wa rais kwa miezi 10 na kuutaja kuwa ni "mapinduzi ya katiba."

Vilevile Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) imeitaka serikali ya Senegal kurejesha ratiba ya awali ya uchaguzi kama ilivyokuwa imepangwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live