Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Senegal: Sall awaonya wagombea kutojitangazia ushindi

Sijutii Uamuzi Wa Kujaribu Kuchelewesha Uchaguzi Wa Senegal: Sall Senegal: Sall awaonya wagombea kutojitangazia ushindi

Mon, 25 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais anayemaliza muda wake wa uongozi nchini Senegal Macky Sall amewaonya wagombea wa kiti cha urais kuacha kudai kuwa washindi wa uchaguzi huo kabla ya Tume ya Taifa ya nchi hiyo kutangaza matokeo rasmi ya uchaguzi.

Macky Sall ambaye hakugombea tena kiti cha urais Senegal amesema mgombea au kambi yoyoye ya kisiasa havipasi kujitangazia ushindi, bali ni vituo vya kupigia kura ndivyo vitatangaza matokeo ya mwisho. Wagombea 17 wa urais walichuana katika uchaguzi wa rais wa jana kumrithi Sall.

Zaidi ya raia milioni 7 wa Senegal walijiandikisha kama wapiga kura katika uchaguzi wa rais wa mwaka huu ambao ulicheleweshwa kwa mwezi mmoja kufuatia mivutano iliyojitokeza.

Mapema Februari, Sall alitangaza kuahiridha uchaguzi huo uliokuwa umepangwa kufanyika Februari 25, lakini Baraza la Katiba la nchi hiyo likaamuru uchaguzi huo ufanyike kabla ya Macky Sall kuondoka madarakani Aprili 2 mwaka huu.

Hii ni katika hali ambayo wafuasi wa mgombea urais wa Senegal, Bassirou Diomaye Faye wamemiminika kwenye barabara za mji mkuu wa nchi hiyo Dakar, kusherehekea ushindi wa mgombea wao huku matokeo ya awali ya uchaguzi wa jana Jumapili yakionyesha kuwa mgombea huyo wa kambi ya upinzani anaongoza. Mgombea anayedaiwa kuongoza, Bassirou Diomaye Faye

Sherehe hizo zimefanyika huku wagombea wasiopungua watano kati ya 19 katika kinyang'anyiro hicho wakitoa taarifa za kumpongeza Faye kwa kile walichokiita ushindi wake kwenye uchaguzi huo.

Lakini mpinzani wake mkuu kutoka muungano tawala ambaye pia ni Waziri Mkuu wa zamani, Amadou Ba, amesema kuwa, sherehe hizo zimefanyika kabla ya wakati wake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live