Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Senegal: Rais Sall kuondoka madarakani muhula wake utakapotamatika

Rais Wa Senegal Ashinikizwa Kufuta Hatua Ya Kuahirisha Uchaguzi Senegal: Rais Sall kuondoka madarakani muhula wake utakapotamatika

Fri, 23 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Senegal, Macky Sall, amesema ataondoka madarakani wakati muhula wake utakapotamatika April 2 mwaka huu, hata hivyo akashindwa kutaja tarehe nyingine ya kufanya uchaguzi.

Kwa mujibu wa rais Sall, tarehe ya uchaguzi itategemea mdahalo wa kitaifa uliopangwa kuanza siku ya Jumatatu, ambao unajumuisha mashirika ya kiraia, vyama vya siasa na wagombea mbalimbali.

Kauli ya mkuu wa nchi imeonekana kupunguza hofu kwamba alikuwa akipanga kuongeza muda wake haswa wakati huu kunaposhuhudiwa mzozo wa kisiasa.

Rais Sall amekuwa chini ya shinikizo la kutangaza tarehe ya uchaguzi tangu atangaze kuuchelewesha kwa zoezi hilo.

Mkuu huyo wa nchi alisema alichukua hatua hiyo ya kuahirisha uchaguzi hadi Desemba ilikutoa nafasi kwa mizozo kuhusu uhalali wa wagombea wengine kutatuliwa.

Lciha ya hatua hiyo mahakama kuu ya nchi hiyo ilisema ilikuwa ni kinyume cha katiba, na kutaka uchaguzi ufanyike haraka iwezekanavyo.

Kauli yake hata hivyo imepokelewa kwa mshangao na wadau wa uchaguzi waliohoji kwa nini hajatangaza tarehe nyingine baada ya kuahirisha uchaguzi uliokuwa ufanyike Jumapili ya wiki hii.

Tayari wanasiasa wa upinzani wamekosoa kauli ya Macky Sall, wakijiandaa kwa maandamano zaidi kushinikiza uchaguzi kufanyika kabla ya muhula wake kutamatika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live