Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Senegal : Mwanafunzi ameuawa kwenye maandamano

Ecowas Senegal Senegal : Mwanafunzi ameuawa kwenye maandamano

Sat, 10 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nchini Senegal, Wizara ya usalama imesema, mwanafunzi ameuawa kwenye maandamano ya upinzani katika mji wa Saint-Louis yaliyofanyika siku ya Ijumaa, kulaani hatua ya rais Macky Sall, kuahirisha uchaguzi hadi mwezi Desemba.

Wakati wa maandamano hayo, polisi walitumia mabomu ya kutoa machozi kuwasambaratisha waandamanaji wenye hasira waliopambana na maafisa wa usalama kwa mawe.

Polisi hawakuruhusu kufanyika kwa maandamano hayo,yaliyogeuka kuwa na fujo, huku waandamanaji wenye hasira, wakiteketeza moto matairi kwenye mji huo ulio Kaskazini mwa nchi hiyo.

Kulikuwa na maandamano mengine katika mji wa Nioro du Rip, umbali wa Kilomita 250 kutoka jiji kuu Dakar ambapo polisi pia walitumia mabomu ya machozi kuwasambaratisha waandamanaji.

Wanasiasa wa upinzani, mashirika ya kiraia na wapinzani wengine wa rais Sall, wamekasirishwa na hatua ya Sall kuahirisha uchaguzi huo kwa kile alichosema kulikuwa na mvutano kati ya bunge na Mahakama ya Katiba kuhusu orodha ya wagombea wa urais.

Mataifa ya Magharibi yakiongozwa na Marekani lakini pia Umoja wa Ulaya, yamelaani hatua ya kuahirishwa kwa uchaguzi na kusema, inatikitisa demokrasia ya Senegal ambayo kwa kipindi kirefu imeonekena thabiti miongoni mwa nchi za Afrika Magharibi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live