Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Senegal: Mkutano wa upinzani kumteua mgombea urais umepigwa marafuku

Serikali Yavunja Chama Cha Upinzani Senegal Senegal: Mkutano wa upinzani kumteua mgombea urais umepigwa marafuku

Sat, 30 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mamlaka nchini Senegal imepiga marufuku mkutano wa kumteua kiongozi wa upinzani anayetumikia kifungo jela Ousmane Sonko kugombea katika uchaguzi wa urais wa 2024, kwa mujibu wa afisa kwenye taifa hilo.

Sonko mwenye umri wa miaka 49 amekuwa katikati ya mzozo na serikali ya taifa hilo ambao umedumu kwa zaidi ya miaka miwili na kuzua matukio kadhaa ya machafuko mabaya yaliotokona na maandamano ya wafuasi wake waliokuwa wanapinga kukamatwa kwa kiongozi wao.

Sonko alikuwa amewasilisha azma yake ya kugombea katika baraza la katiba ili kushiriki uchaguzi wa Februari licha ya serikali kukataa kumpa stakabadhi muhimu za kushiriki zoezi hilo.

Kwa mujibu wa barua iliyotiwa saini na gavana wa Dakar, Cherif Mouhamadou Blondin Ndiaye, mkutano wa Jumamosi ulipigwa marufuku kutokana na kile ambacho mamlaka imesema ni kumekuwepo na hofu ya kuvuruga utulivu wa umma, kuhitilifiana na usafirishaji huru wa watu na bidhaa.

El Malick Ndiaye, msemaji wa chama kilichofutwa cha Sonko Pastef, kupitia ukurasa wa facebook, alikashifu hatua hiyo ya serikali kuzuia mkutano huo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live