Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Senegal: Kuahirishwa uchaguzi njama dhidi ya Waziri Mkuu?

Senegal Waziri Mkuu.png Senegal: Kuahirishwa uchaguzi njama dhidi ya Waziri Mkuu?

Tue, 6 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nchini Senegal, hali imekuwa mbaya sana kwa Waziri Mkuu Amadou Ba tangu Jumamosi Februari 3. Hakika, alikuwa mgombea wa serikali katika uchaguzi wa urais mnamo Februari 25 na alikuwa akipinga kuahirishwa kwa uchaguzi huo.

Leo hii baada ya kutangazwa kuahirishwa bado anaweza kubaki kuwa Waziri Mkuu? Hadi Jumamosi, mkurugenzi wa zamani wa vyombo vya habari Mamoudou Ibra Kane alimfanyia kampeni mkuu wa vuguvugu la "Kesho ni sasa". Akihojiwa na mwandishi wetu Christophe Boisbouvier, mkurugenzi mkuu wa zamani wa kundi la Futur Media anatambua kuwa uhusiano kati ya wakuu hao wawili wa serikali ya Senegal hauko katika hali nzuri tena...

Wabunge nchini Senegal wamepitisha muswada wa kuahirisha uchaguzi wa rais hadi Desemba 15, mwaka huu wa 2024 na kuongeza mamlaka zaidi kwa rais anayemaliza muda wake Macky Sall, hatua iliyozua vurugu ndani ya bunge hapo jana jijii Dakar.

Muswada huo wa kuahirishwa kwa uchaguzi Mkuu nchini Senegal hadi Desemba 15 mwaka huu wa 2024 ulifikiwa baada ya wabunge walioonekana kuunga mkono utawala wa rais anayemaliza muda wake Macky Sall pamoja na wapinzani kukabiliana.

Maafisa wa polisi walilazimika kuingilia mara moja mvutano huo na kuwatoa nje wabunge wa upinzani, ambao walionekana kutounga mkono tarehe hiyo, na pia kuongezewa mamlaka zaidi kwa rais huyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live