Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Semenya ashindwa rufaa yake Uswisi

F333d71a11280dbd3b52359c67f2e385 Semenya ashindwa rufaa yake Uswisi

Thu, 10 Sep 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MWANARIADHA wa kimataifa wa Afrika Kusini, Caster Semenya, ameshindwa rufaa yake katika Mahakama Kuu ya Uswisi, kupinga zuio la ongezeko la homoni za kiume kwa wanariadha wa kike.

Hivyo, Semenya haruhusiwi kushindana katika mbio za kati ya mita 400 hadi za maili moja bila ya kutumia dawa za kupunguza homoni hizo, kufuatia sheria kubadilishwa na Shirikisho la Kimataifa la Riadha (WA) mwaka 2019. “Nimesikitishwa sana.

Napinga kunizuia mimi kuwa nilivyo,” alisema mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka 29. Shirikisho hilo la riadha liliweka kanuni hiyo kwa wanariadha wa kike wenye homoni zaidi za kiume, ama watumie dawa kupunguza homoni hizo ili waweze kushiriki mbio za uwanjani kuanzia mita 400 hadi maili moja au wakimbie mbio za umbali mwingine.

Wanariadha wenye jinsia mbili wana kiwango kikubwa cha homoni, ambacho WA inaamini kinawawezesha kufanya vizuri zaidi katika mashindano kuliko wenzao.

“Kuwaondoa wachezaji wa kike au kuvuruga afya zetu kwa sababu ya uwezo wetu wa asili unaiweka pabaya WA.” “Kwa kweli nitaendelea kupambana kwa ajili ya haki za binadamu wanawake uwanjani na nje ya uwanja hadi pale wote tutakapoweza kukimbia kutokana na tulivyozaliwa.”

“Najua nini haki na nitafanya yote niwezayo ili kupigania haki za binadamu kwa wasichana mahali kokote,” alisema Semaya.

Mahakama ya Usuluhishi wa Mambo ya Michezo (Cas) mwaka jana ilipinga rufaa ya Semenya dhidi ya kanuni za WA. Mahakama Kuu ya Uswisi kwa muda iliweka kando uamuzi huo, kabla ya baadae kubadili uamuzi wake wa awali.

Hiyo ina maana kuwa, Semenya aliyeshinda medali ya dhahabu katika michezo ya Olimpiki kwenye mbio za mita 800 mwaka 2012 na 2016, alishindwa kutetea ombi lake kuzuia uamuzi wa mabadiliko uliofanywa na WA.

Taarifa ya WA imesema uamuzi huo una maana kuwa, Semenya hataweza kutetea taji lake la mita 800 katika michezo ya Olimpiki ya 2020 itakayofanyika Tokyo, Japan mwakani.

Machi, mwaka huu, Semanya alisema anataka kushindana katika mbio za mita 200 Tokyo, ambazo hazihitaji kutumia dawa za kupunguza nguvu za homoni.

Ili kushindana, Semenya anatakiwa kwanza kufuzu kwa kutumia muda wa 22.80, ingawa muda wake wa sasa ni sekunde 24.26

Chanzo: habarileo.co.tz