Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sekta ya utalii yapata hasara ya Tsh. Trilioni 11, ajira milioni mbili

EAC TOURISM Sekta ya utalii yapata hasara ya Tsh. Trilioni 11, ajira milioni mbili

Tue, 24 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Soko la utalii kwenye nchi za Afrika Mashariki limepata hasara ya Dola Bilioni 4.8 (Zaidi ya Tsh. Trilioni 11) pamoja na kupoteza ajira milioni mbili kwenye sekta hiyo kwa mwaka 2020 kutokana na kusambaa kwa ugonjwa wa Corona.

Kwa mujibu wa ripoti ya “Uchunguzi wa EABC juu ya Athari za Covid-19 kwenye Sekta zilizochaguliwa: Sekta ya Utalii na Ukarimu na Sekta ya Uzalishaji Mwanga na Kilimo na Usalama wa Chakula” imeonesha kuwa takribani watalii milioni 4.2 walishindwa kusafiri kufika kwenye maeneo yao ya utalii kwenye nchi za Afrika Mashariki.

Athari hizo zimesababisha hasara pia kwenye sekta nyingine zinazoshirikiana na sekta ya utalii kupelekea kushukwa kwa uchumi na kupoteza pesa za kigeni. Ikumbukwe kwamba sekta ya utalii ndio inayoongoza kwa kuingiza pesa za kigeni kwenye ukanda wa Afrika Mashariki.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live