Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sehemu ya uwanja wa ndege Nairobi yafungwa baada ya kutokea

Sehemu Ya Uwanja Wa Ndege Nairobi Yafungwa Baada Ya 'moto Mdogo' Kutokea Sehemu ya uwanja wa ndege Nairobi yafungwa baada ya 'moto mdogo' kutokea

Mon, 25 Mar 2024 Chanzo: Bbc

Sehemu ya uwanja mkuu wa ndege nchini Kenya imefungwa kwa muda baada ya tukio la moto.

Hitilafu ya umeme ilisababisha tukio la "moto mdogo" katika Kituo cha 1E cha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta Jumatatu asubuhi, Mamlaka ya Viwanja vya Ndege vya Kenya (KAA) ilisema katika taarifa.

"Hali ilidhibitiwa haraka, bila majeraha au majeruhi kutokana na tukio hilo."

Umeme kwenye kituo cha umeme umezimwa kwa muda kama hatua ya tahadhari na shughuli zote za kuwasili kwa ndege zimeelekezwa kwenye Kituo cha 1A, KAA ilisema.

Tukio hilo lilizua taharuki huku abiria na wafanyakazi wakitolewa katika eneo lililoathiriwa.

Chanzo: Bbc