Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Saudi Arabia yashutumu shambulizi dhidi ya ubalozi wake Sudan

Saudi Arabia Yashtumu Shambulizi Dhidi Ya Ubalozi Wake Huko Sudan Saudi Arabia yashutumu shambulizi dhidi ya ubalozi wake Sudan

Thu, 8 Jun 2023 Chanzo: Bbc

Saudi Arabia imeshtumu shambulio dhidi ya ubalozi wake katika mji mkuu wa Sudan "kwa maneno makali".

Wizara ya mambo ya nje ya Saudia ililaumu makundi yenye silaha kwa kuvamia na kuharibu jengo la Khartoum, na kuongeza kuwa mali na nyumba za wafanyakazi wa Saudi pia zimeharibiwa.

Saudi Arabia pamoja na Marekani, zimechukua uongozi katika kujaribu kujihusisha na pande zinazozozana tangu mzozo huo ulipozuka katikati ya mwezi Aprili.

Ufalme huo ulikataa kabisa "aina zote za ghasia na uharibifu dhidi ya ujumbe wa kidiplomasia na uwakilishi", taarifa ya wizara ya mambo ya nje ilisema.

Pia ilisisitiza umuhimu wa kukabiliana na makundi ambayo ilisema yanajaribu kudhoofisha urejeshwaji wa utulivu na usalama nchini Sudan.

Taarifa hiyo iliyochapishwa kwenye Twitter, haikubainisha ni makundi gani yalihusika na shambulio hilo.

Pande zinazopigana zinahusisha jeshi la Rapid Support Forces (RSF) - wawili hao wakitofautiana tangu kuchukua mamlaka kwa pamoja katika mapinduzi ya Oktoba 2021.

Vyombo vya habari vya Saudi vimejaribu kudumisha msimamo wa kutoegemea upande wowote katika kuangazia mzozo huo.

Siku ya Alhamisi, tovuti ya habari ya Saudia Al Arabiya iliripoti kuwa mwezi uliopita jeshi lilisema haliwezi tena kutoa ulinzi kwa balozi za kidiplomasia, likiishutumu RSF kwa kushambulia balozi.

Hadi wiki iliyopita, Saudi Arabia ilikuwa ndio mwenyeji wa mazungumzo ya kusitisha mapigano huko Jeddah kati ya wapinzani.

Makubaliano ya kulinda haki za binadamu yaliyokiukwa mara kwa mara, yaliyoanza tarehe 22 Mei, yalimalizika rasmi Jumamosi jioni.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani alikuwa katika mji mkuu wa Saudi, Riyadh, siku ya Jumatano ambapo nchi hizo mbili ziliahidi tena kuendeleza juhudi za kusitisha mapigano ambayo sasa yameingia katika wiki ya saba.

Chanzo: Bbc