Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sasa si wakati wa mazungumzo - mkuu wa jeshi la Sudan

Sasa Si Wakati Wa Mazungumzo   Mkuu Wa Jeshi La Sudan Sasa si wakati wa mazungumzo - mkuu wa jeshi la Sudan

Tue, 29 Aug 2023 Chanzo: Bbc

Mkuu wa jeshi la Sudan kwa mara nyingine amefutilia mbali mazungumzo na kikosi cha Rapid Support Forces (RSF) ili kumaliza mzozo wa miezi minne nchini mwake ambao umesababisha vifo vya maelfu ya watu na wengine kuikimbia nchi na makazi yao.

Jenerali Abdel Fattah al-Burhan yuko nchini Misri kwa mazungumzo naRais Abdel Fattah al-Sisi.

Hii ni safari ya kwanza ya jenerali huyo nje ya nchi tangu vita kuanza.

Lakini alizima uvumi wowote kwamba hii ilikuwa hatua ya kwanza kuelekea juhudi mpya za kutatua mapigano.

Jenerali Burhan aliwaambia waandishi wa habari nchini Misri:

"Kundi hili (RSF) si kama watu wetu nchini Sudan. Hatuna la kuwaambia, na sasa sio wakati wa mazungumzo, tunajitolea wakati wetu wote kwa vita hivi, tunajitolea kumaliza uasi huu.’’

Aliongeza kuwa: ‘’Tunalenga kumaliza kipindi hiki na kutoka ndani yake tukiwa na nguvu, thabiti na tukiwa tumeinua vichwa vyetu juu."

Chanzo: Bbc