Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sanamu inayotabasamu yafukuliwa Misri

Sanamu Inayotabasamu Yafukuliwa Misri Sanamu inayotabasamu yafukuliwa Misri

Tue, 7 Mar 2023 Chanzo: Bbc

Wanaakiolojia wamegundua sanamu inayofanana na sfinksi karibu na Hekalu la Hathor, mojawapo ya maeneo ya kale yaliyohifadhiwa vyema nchini Misri.

Inaaminika kwamba uso wa sanamu hiyo ya sfinksi unawakilisha mfalme wa Kirumi Claudius.

Sanamu iliyogunduliwa ni ndogo zaidi kuliko ile maarufu ya Sfinksi kwenye mapiramidi ya Giza, ambayo ina urefu wa mita 20 (futi 66).

Vitu hivyo vya kale vilipatikana ndani ya kaburi la ngazi mbili kwenye Hekalu la Dendera huko Qena, kilomita 450 kusini mwa mji mkuu, Cairo.

Mtawala Klaudio, ambaye wanaakiolojia wanaamini kuwa tabasamu ya sanamu hiyo inaweza kuwa yake, alipanua utawala wa Kirumi hadi Afrika Kaskazini kati ya 41 na 54 AD.

Wanaakiolojia watachunguza alama kwenye bamba la mawe, ambayo inaweza kufichua habari zaidi juu ya utambulisho wa sanamu hiyo, wizara ilisema.

Kando ya sanamu hiyo ya sfinksi "iliyochongwa kwa uzuri na kwa usahihi," wanaakiolojia pia walipata jiwe la enzi ya Warumi na maandishi ya kale ya michoro ya Misri.

Kaburi la chokaa linajumuisha jukwaa la safu mbili na matofali ya enzi ya Byzantine.

Chanzo: Bbc