Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Samatta uso kwa uso na Guardiola

97555 Samatta+pic Samatta uso kwa uso na Guardiola

Mon, 2 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

London, England. Mbwana Samatta amesema anataka kuweka historia kwenye Uwanja wa Wembley, London.

Samatta leo ataiongoza Aston Villa katika mchezo wa fainali ya Kombe la Ligi dhidi ya Manchester City inayonolewa na kocha Pep Guardiola.

“Sijawahi kucheza Wembley. Hii ni nafasi ambayo kila mchezaji anayechipukia katika soka atakuwa anaiota, ni mchezo mgumu dhidi ya timu bora,” alisema Samatta.

Tangu ajiunge na Aston Villa, Samatta amefunga bao moja katika mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Bournemouth ambao walipoteza kwa kufungwa mabao 2-1 ugenini.

Kabla ya kutua England, Samatta ambaye leo atashuhudiwa uwanjani na baba yake Ally Samatta, ataongoza safu ya ushambuliaji katika kikosi cha Aston Villa.

Mchezaji huyo wa zamani wa Simba, alisema alikuwa akivutiwa na kiwango bora cha washambuliaji waliotamba katika Ligi Kuu England akiwemo nahodha wa zamani wa Arsenal na Ufaransa Thierry Henry.

Pia Soma

Advertisement

Chanzo: mwananchi.co.tz