Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Salva atangaza kuwaita viongozi wa Sudan kutatua mzozo

Sheria Ya Uchaguzi Ya Sudan Kusini Yawafanya Wabunge Kuandamana Salva atangaza kuwaita viongozi wa Sudan kutatua mzozo

Tue, 17 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir amesema atawaalika wawakilishi wa viongozi wa kisiasa wa Sudan katika mji mkuu wa Juba katika jitihada za kumaliza mzozo wa miezi sita.

Taarifa kutoka kwa kitengo cha wanahabari cha Kiir inasema mkutano huo utafanyika wiki ijayo, lakini haijataja ni nani watahudhuria.

Kiir alitoa wito kwa viongozi wa kijeshi na kisiasa nchini Sudan kumaliza mzozo unaoendelea kupitia mazungumzo ya amani.

Mshauri wa usalama wa kitaifa wa rais wa Sudan Kusini, Tut Gatluak Manime, anasema viongozi wa Sudan watapitia mkataba wa amani wa Juba uliotiwa saini mwaka 2020 kati ya serikali ya mpito ya wakati huo na makundi ya waasi kama sehemu moja ya kutatua mgogoro uliopo.

Jeshi la Sudan limekuwa likipigana na washirika wake wa zamani, Kikosi cha RSF tangu mwezi Aprili.

Maelfu wameuawa na zaidi ya watu milioni tano wamekimbia makazi yao, kulingana na taarifa ya UN. Mzozo huo umeingia mwezi wa sita sasa.

Wachambuzi wa masula ya kimataifa wanaamini kuwa rais Kiir yuko katika nafasi nzuri ya kuwa mpatanishi kati ya wapinzani wa Sudan.

Mwezi Juni, IGAD ilimteua rais wa Kenya William Ruto kuongoza timu ya upatanishi wa pande nne kutatua mzozo wa Sudan.

Jeshi la Sudan lilikataa mpango huo unaoongozwa na Kenya, likimtuhumu Ruto kwa kuegemea upande wa RSF, madai ambayo Kenya ilikanusha.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live